Isaiah 49:3-6

3 aAkaniambia, “Wewe u mtumishi wangu,
Israeli, ambaye katika yeye
nitaonyesha utukufu wangu.”
4 bLakini nilisema, “Nimetumika bure,
nimetumia nguvu zangu bure bila faida.
Hata hivyo linalonistahili liko mkononi mwa Bwana,
nao ujira wangu uko kwa Mungu wangu.”

5 cSasa Bwana asema:
yeye aliyeniumba tumboni kuwa mtumishi wake,
kumrudisha tena Yakobo kwake
na kumkusanyia Israeli,
kwa maana nimepata heshima machoni pa Bwana,
naye Mungu wangu amekuwa nguvu yangu;
6 dyeye asema:
“Je, ni jambo dogo sana wewe kuwa mtumishi wangu
ili kurejeza makabila ya Yakobo,
na kuwarudisha wale Waisraeli niliowahifadhi?
Pia nitakufanya uwe nuru kwa ajili ya watu wa Mataifa,
ili upate kuleta wokovu wangu hata miisho ya dunia.”
Copyright information for SwhNEN